Burkina Faso yawafukuza wanadiplomasia watatu wa Ufaransa kutokana na "shughuli za uasi"

Baada ya kutangaza kuwa "watu wasiofaa" kwa "shughuli za uasi" na mamlaka ya Burkina Faso, wanadiplomasia watatu wa Ufaransa wametakiwa kuondoka nchini Burkina Faso, kulingana na barua iliyoandikwa siku ya Jumanne na kutumwa kwa ubalozi wa Ufaransa. Uhusiano kati ya Paris na Ouagadougou umezorota sana tangu Kapteni Ibrahim Traoré aingie mamlakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi wa Septemba 2022.

Ufaransa - waliodaiwa kuwa maafisa wa ujasusi na mamlaka ya Burkina Faso, mafundi wa matengenezo ya kompyuta kulingana na chanzo cha kidiplomasia cha Ufaransa - walikamatwa huko Ouagadougou, kufunguliwa mashtaka na kisha kufungwa, kulingana na chanzo kutoka Ufaransa.

Leo wako chini ya kizuizi cha nyumbani, kulingana na vyanzo vya usalama nchini Burkina Faso.

Nchini Burkina Faso pekee, vita na wanajihadi vimesababisha vifo vya raia na wanajeshi 20,000 na takriban watu milioni mbili wamekimbia makazi yao tangu mwaka 2015.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii