Ulaya yaiwekea vikwazo vipya Iran baada ya kulipiza kisasi

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuweka vikwazo vipya kwa watengenezaji wa ndege zisizo na rubani na makombora wa Iran kutokana na shambulio la kulipiza kisasi dhidi ya Israel mwishoni mwa juma lililopita.


Akizungumza katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel alisema vikwazo hivyo ni ujumbe wa wazi waliokuwa wanautuma kwa Iran kwa kuyalenga makampuni yanayotengeneza zana hizo. 

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema nchi yake ingeliamua jinsi ya kujibu mashambulizi ya Iran, licha ya mataifa yenye nguvu duniani kuiitka kujizuia ili kuepusha kutanuka kwa mgogoro wa Mashariki ya Kati.

Umoja wa Ulaya ulikuwa tayari umeiwekea Iran vikwazo kutokana na usambazaji wake wa ndege zisizo na rubani kwa Urusi, lakini vikwazo hivyo vimekuwa na athari ndogo katika kukata uhusiano kati ya Tehran na Moscow.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii