Wanafunzi kadhaa wakamatwa wakiandamana kupinga vita Gaza

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Columbia kilichopo jijini New York, wamemakamatwa na polisi baada kuanzisha maandamano ya kulaani vita vinavyoendelea kwenye ukanda wa Gaza.

Polisi wamewamia wafunzi hao waliokuwa wamejifungia kwenye ukumbi wa Hamilton, kwenye chuo na kuwakamata.

Kabla ya hatua hiyo, mamia ya wanafunzi walikuwa wafunga barabara za kuingia kwenye chuo hicho, na kuapa kuendeleza maandamano hayo,; hadi pale mashambulio kwenye ukanda wa Gaza, yatakapokoma.

Uongozi wa Chuo hicho, umesema waandamanaji waliovamia ukumbi huo sio wanafunzi wa taasisi hiyo ya elimu na hivyo kuomba maafisa wa usalama kusaidia kuwaondoa.

Aidha, wanafunzi walioingia kwneye ukumbi huo wametishiwa kufukuzwa chuoni, huku rais Joe Biden alilaani kile alichosema maandamano yasiyokuwa na amani baada ya kushuhudiwa uharibifu na makabiliano na maafisa wa polisi.

Mbali na Chuo Kikuu cha Columbia, wafunzi kwenye vyuo vikuu vingine nchini Marekani na hata Ufaransa kwa siku kadhaa zilizopita, wamekuwa wakiandamana kuwaunga mkono Wapalestina.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii