logo
  • Nyumbani
  • HABARI ZOTE
  • Habari
    • KITAIFA & KIMATAIFA
    • BIASHARA & UCHUMI
  • Siasa
  • Michezo
  • Burudani
    • BURUDANI ZOTE
    • JEMBE INTERVIEW
  • Zaidi
    • MAGAZETI YA LEO
    • MAKALA
    • VIDEO
    • MATUKIO
    • JEMBE FM TEAM
    • PARTNERS
BREAKING   
Sikiliza Jembe FM Radio Online . . .
DEVELOPING
Sikiliza Jembe FM Radio Online . . .

Soma Habari Husika

  • Habari Nzima Kwa Ujumla

Ukimtukana Mtu Mtandaoni Jela Mwaka Mmoja

  • Na Asha Business
  • June 14, 2022

Bunge la Japan limepitisha mswada wa sheria mpya ya kudhibiti matusi mitandaoni ambayo inatarajiwa kusainiwa na Rais wa nchi hiyo ambayo inatoa hukumu ya mwaka mmoja jela au faini ya Yen 300,000 ambayo ni sawa na dola 2,200.

Sheria hii ni marekebisho ya sheria iliyopita kuhusu masuala ya udharirishaji na matusi mitandaoni ambayo ilikuwa inatoa adhabu ya kuzuiliwa kutumia huduma hiyo kwa muda wa siku 30 pamoja na faini ya Yen 10,000 ambayo ni sawa na dola 75.

Mswada huo umeleta mgawanyiko wa mawazo na mitazamo miongoni mwa wananchi wa Japan baadhi wakisema kuwa itazuia uhuru wa kuongea na kujieleza na wengine wanaoafiki wakisema itasaidia kupunguza udharirishaji na matusi ya mitandaoni.

 

Kwa mujibu wa Msemaji kutoka Wizara ya Sheria, sheria hii ya matusi mtandaoni inatofautiana na sheria ya kumchafua mtu (Defamation).

 

Mwanasheria wa makosa ya jinai kutoka nchini Japan Seiho Cho ameonya kuwa sheria hii mpya haitoa ufafanuzi ni lipi hasa kosa linalotafsiriwa kama udharirishaji.

“Kulikuwa na ulazima wa kuwepo muongozo unaothibitisha lipi ji tusi.

“Kwa mfano kwa sasa kama atatokea mtu akamuita kiongozi wa Japan mjinga, pengine kwa sheria hii mpya iliyofanyiwa marekebisho inaweza kutambulika kama tusi.” Alisema Cho.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii

  • Follow Us

  • Follow Us

  • Follow Us

  • Subscribe

Unaweza Penda Hizi
ad

Ajiua kwa kujinyonga kwenye banda la mbuzi Manyara

ad

Polisi Morogoro wachunguza kifo dada wa kazi, magari kuchomwa moto Mvomero

ad

Mvua kubwa yaezua paa la nyumba Mtwara

ad

Maafisa uhamiaji 3 wahukumiwa kunyongwa mpaka kufa

ad

Uzembe ndiyo chanzo cha ajali iliyoua 5 Songwe

ad

RC Mhita akagua athari za mvua Shinyanga

Matawi Yetu
  • Jembe Group
  • Jembe Development
  • Jembe Beach
  • Jembe Digital
  • Jembe DJ
  • Jembe Stage And Sound
  • Jembe Events
  • Jembe Ni Jembe Team

Habari Zaidi

  • Ajiua kwa kujinyonga kwenye banda la mbuzi Manyara

    • saa moja lililopita
  • Familia za waathiriwa wa maandamano kuandamana hadi ikulu ya rais kudai haki

    • saa moja lililopita
  • Rwanda Yafunga Zaidi ya Makanisa 10,000 ya Kiinjili kwa Ukiukwaji wa Sheria

    • 3 masaa yaliopita

Habari Category

  • Habari Zote
  • Siasa
  • Michezo
  • Burudani
  • Habari Ndani Na Nje
  • Video
  • Uchumi Na Biashara
  • Magazeti
  • Makala

Wasiliana Nasi

JEMBE NI JEMBE GROUP ,
P. O. Box 1334,
PLOT NO.111/BLOCK "A"
HOUSE No:43 MAKONGORO STREET,
ILEMELA MWANZA - TANZANIA

info@jembenijembe.com

+ 255-786-385-475 ,
+ 255-716-385-475.

  • PRIVACY POLICY
  • TERMS AND CONDITIONS
  • STAFF LOGIN

POWERED BY

© Jembe Ni Jembe Companies.

Created And Maintained By XFoundationCode