Mo Dewji Atoa Tamko Zito Kuhusu Simba -”Kusema Sitoi Hela Ni Fitina Nimewekeza Bilioni 87

Mwekezaji maarufu na Rais wa heshima wa klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji (Mo), amevunja ukimya kwa kutoa ufafanuzi mzito kuhusu mchango wake ndani ya klabu hiyo tangu alipoanza kuwekeza rasmi mwaka 2017.

Kupitia kauli yake ya wazi, Mo Dewji amesema kuwa kati ya mwaka 2018 hadi sasa, tayari amewekeza jumla ya shilingi Bilioni 87, fedha zilizotumika katika maeneo mbalimbali ya maendeleo ya klabu, ikiwemo uendeshaji, usajili, mishahara ya wachezaji, na misaada ya dharura.

“Kuanzia mwaka 2018 hadi leo, nimewekeza shilingi Bilioni 45 kwa ajili ya mishahara, usajili, maandalizi ya timu na mahitaji mengine ya uendeshaji,” alisema Mo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii