Mwanamitindo na sosholaiti maarufu kutoka Kenya, Vera Sidika, anayejulikana kwa jina la utani kama Vee Beiby, ameibuka upya na kuteka mitandao ya kijamii kwa kishindo baada ya kuanika sura mpya ya maisha yake ya kifahari.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera aliwatangazia mashabiki wake kuwa ameanza kipindi kipya cha maisha, kilichojaa mitindo, madaha na mshawasha wa hali ya juu. Akiwa amepiga picha kwenye gari lake jipya aina ya Range Rover, Vera aliandika kwa mbwembwe:
“New wheels, new feels, new chapter. It’s Vera Sidika 2.0 & I’m in love with this new era. #RichBitch #VeeMoney #CashMadam”
Ameitaja gari hiyo kama “mnyama” mwenye nguvu na umbo la kuvutia, akisema ni zawadi ya kujipongeza kwa mafanikio yake.
Wafuasi wake wengi hawakusita kuonyesha furaha na pongezi, wakisema Vera Sidika amerudi kwa nguvu mpya na mvuto wa kipekee.
Huu ni mwanzo wa kipindi kipya kwa Vera kipindi cha uhuru, mafanikio na kujiamini. Ameonyesha kuwa bado ni malkia wa maisha ya kifahari, na hakuna kinachomzuia kurudi kileleni.