Rapa maarufu kutoka Memphis, GloRilla avunja ukimya

Rapa maarufu kutoka Memphis, GloRilla, hatimaye amezungumza hadharani kufuatia kukamatwa kwake hivi karibuni kwa tuhuma za kumiliki dawa za kulevya, na kwa mujibu wa maelezo yake, kosa kubwa si dawa bali jinsi tukio hilo lilivyoshughulikiwa na mamlaka husika.

Kupitia mitandao yake ya kijamii siku ya jana  Alhamisi, GloRilla alielezea upande wake wa tukio hilo lililosababisha awekwe kizuizini na kuasema kuwa;

“CRAZY‼️ Nyumba yangu ilivamiwa Jumamosi nikiwa Indianapolis nikitumbuiza kwenye mechi ya WNBA All Star, lakini badala ya kuwasaka waliovamia, wameamua kushughulika na bangi,” aliandika kwenye ukurasa wake wa "X"“1. Kwa hiyo hapana, sikukamatwa

2. Nyumba yangu iliivamiwa

3. Sikuwepo nyumbani,” 

“Kwa ufupi, nyumba yangu yavamiwa halafu mimi ndiye nakamatwa. Basi hiyo ndiyo tea ,” aliandika

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 24 alifafanua kuwa hakuwepo kabisa Georgia wakati uvamizi huo ulipotokea. Kwa mujibu wa taarifa za awali, polisi waliitwa nyumbani kwa GloRilla kufuatia tukio hilo la wizi, ambapo walidaiwa kugundua dawa za kulevya aina ya controlled substance. Hata hivyo, maelezo kuhusu uhalali wa upekuzi na kukamatwa kwake bado hayajajulikana wazi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii