Mtanzania Juma Hamad maarufu kama Jayzow ameshinda tuzo ya Kimataifa katika tuzo za GMA ( Ghana Merit Awards 2025 ) zilizofanyika Nchini Ghana
Jayzow ameibuka mshindi katika kipengele cha Meneja Bora Wa Vipaji kupitia hafla ya ugawaji tuzo hizo zilizofanyika katika ukumbi wa GNAT Hall huko Adabraka, Accra Nchini Ghana
Tuzo hizo zinalenga kutambua mchango wa kazi kutoka kwenye makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo Tasnia ya burudani ambapo kwa mwaka huu tuzo hizo zilijumuisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Marekani pamoja na Ulaya
Meneja Jayzow ameshiriki kusimamia kazi za wasanii mbalimbali hapa Nchini akiwa kama Meneja lakini pia Meneja Mradi ambapo amefanya kazi na wasanii kama Conboi Cannabino,Maua Sama,Kusah,Jaiva,Chino na wengine wengi
Ushindi huu sio tu wa mtu binafsi bali pia ni ushindi kwa Taifa la Tanzania haswa katika kuchochea maendeleo ya Muziki na burudani kwa ujumla