Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amezindua rasmi uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu ujulikanao kama Nsekela Stadium uliojengwa na Abdulmajid Nsekela Mwenyekiti wa Taasisi ya Abdulmajid Nsekela Foundation.
Akizindua uwanja huo uliojengwa wilayani Kyerwa katika eneo la Rwenkorongo, Mkuu wa Mkoa Mwassa amempongeza Abdulmajid Nsekela mzaliwa wa Kyerwa kutekeleza kwa vitendo wito wake wa "Ijuka Omuka" kwa kukumbuka nyumbani na kuwekeza katika mradi mkubwa unaokwenda kuinufaisha jamii ya Wanakagera.
"Uwanja huu nauangalia kwa jicho la tatu wananchi wa Wilaya ya Kyerwa wamepata fursa ya kufanya mazoezi wakiwemo wanafunzi wa shule jirani hapa, pia taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi aidha kupitia mashindano mabalimbali tutaweza kupata burudani hapa badala ya kwenda mbali na Wilaya yetu," alisema Mwassa.