Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura kuidhinisha usitishwaji wa vita na kuruhusu misaada kuingia Gaza, licha ya kura turufu ya Marekani ambayo haiungi mkono hatua hiyo.
Wanachama 10 wasiokuwa wa kudumu wa baraza hilo walianzisha mchakato wa kusitishwa kwa vita eneo la Gaza mwishoni mwa mwezi uliopita, baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza kuwepo kwa baa la njaa eneo hilo kutokana na vita vya miaka miwili.
Rasmu ya mapendekezo hayo inajumuisha kuondoa vikwazo vya kutoa misaada na kusitishwa kwa vita mara moja, ila vyanzo vya habari vinasema kwamba mataifa ya Ufaransa, Uingereza na Urusi, yameonyesha wasiwasi wao kuhusu, kiwango cha misaada kinachoelekezwa Gaza na Umoja wa Mataifa, kiwango ambacho Marekani imekuwa ikipinga na kutetea mshirika wake Israeli.
Wacahama wengine 14 wa baraza hilo la Umoja wa Mataifa wamekuwa wakieleza masitiko yao, kuhusiana na Marekani kuendelea kutumia kura ya turufu kupinga usitishwaji wa vita kule Gaza, Umoja wa mataifa nao ukiituhumu Isreali kwa kutekeleza uhalifu wa kivita kule Gaza na kutaka kumaliza Wapelestina.