Waisrael wanajiandaa kuomboleza waliouawa, wakati taifa hilo linaadhimisha miaka miwili tangu shambulio la Hamas la Oktoba 7, ambalo liliingiza eneo hilo katika vita vya maangamizi.
Katika kumbukumbu ya miaka miwili tangu mauaji ya Oktoba 7 yaliyofanywa na Kundi la Hamas nchini Israel, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kusitisha vita vya Gaza. Kiongozi huyo amenukuliwa akisisitiza: "Sitisheni uhasama katika Gaza, Israel na eneo lote sasa." Guterres aliongeza kuwa pendekezo jipya la Rais wa Marekani Donald Trump linatoa fursa ya kumaliza mgogoro huo ikiwa ni baada ya miaka miwili ya maumivu, ni lazima kufanikishwe matumaini.Oktoba 7, 2023, wapiganaji wa Hamas na makundi mengine ya Kiislamu walitekeleza mauaji mabaya zaidi katika historia ya Israel, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na zaidi ya 250 kutekwa na kupelekwa Ukanda wa Gaza.