Marioo Atoa Kauli Nzito Kuhusu Mke Wake

Msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Marioo, amezua gumzo mitandaoni baada ya kuandika ujumbe mrefu wenye hisia kali kupitia ukurasa wake wa Instagram akimzungumzia mke wake, Paula Kajala, na watu waliokuwa wakimsema au kumpotosha.

Kupitia chapisho hilo, Marioo aliweka wazi kuwa amechoshwa na tabia za baadhi ya watu wanaojaribu kuingilia maisha yake ya ndoa, hasa wale aliowaita waliomshauri mke wangu atoe mimba na wanaomtongoza kisiri.

“Waliomshauri mke wangu atoe mimba, mnaomtongoza, na wale wenye tabia za kimalaya nawaanika hadharani,” ameandika Marioo kwa ukali, akionyesha wazi hisia za kulinda ndoa yake na Paula.

Ujumbe huo umeibua maoni mbalimbali kutoka kwa mashabiki na wadau wa burudani, wengi wakionyesha mshangao huku wengine wakimpongeza kwa kusimama kidete kulinda heshima ya familia yake.

Wengine wameeleza kuwa kauli hiyo inaweza kuwa ishara ya migogoro ya ndani ya ndoa au presha kutoka mitandaoni, hasa ikizingatiwa kuwa wanandoa hao wamekuwa wakifuatiliwa kwa karibu tangu walipooana.

Hadi sasa, Paula Kajala hajatoa tamko lolote rasmi kuhusu maneno ya Marioo, na mashabiki wanasubiri kuona kama ataeleza upande wake wa hadithi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii