Caren Simba Akanusha Madai ya Kutoka Kimapenzi na Pacome Zouzoua

Mrembo wa mitandao ya kijamii Caren Simba (@caren_simba), amefunguka na kufafanua kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua (@pacom_zouzoua) kinyume na taarifa zinazosambaa mitandaoni.

Madai hayo yalianza kuenezwa kupitia mitandao ya kijamii ikihusisha pia jina la video vixen Bongo, Official Nai @officiall_nai jambo lililoibua mjadala miongoni mwa mashabiki Caren amekanusha madai hayo kwa nguvu akisisitiza kuwa taarifa zinazosambaa ni za uongo na hazina uthibitisho wowote.

Kupitia ukurasa wake, Caren amesema:“Sijawahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na Pacome Zouzoua. Tuhimu ni kutafuta ukweli kabla ya kueneza taarifa zisizo sahihi.”

Kauli hii imepokelewa kwa mitazamo tofauti: baadhi ya mashabiki wameshukuru ukweli huo na kumpa Caren sapoti, huku wengine wakisisitiza umuhimu wa kuwa makini na kile kinachosambazwa mtandaoni.

Caren Simba ameendelea kujitambulisha kama mmoja wa warembo maarufu mtandaoni, anayejulikana kwa ucheshi, mitindo, na jinsi anavyokamata mjadala bila kuvunja maadili ya kijamii.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii