CAF Yatangaza Zawadi za Fedha za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetangaza rasmi muundo wa zawadi za fedha kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, itakayofanyika nchini Morocco ambapo michuano hiyo itahusisha mataifa 24 kutoka Afrika, na kwa mara nyingine, CAF imeonyesha dhamira ya kuendeleza kiwango cha michuano hii kwa kutoa zawadi kubwa zaidi kwa timu zitakazofanya vizuri.

Kwa mujibu wa muundo mpya wa zawadi, bingwa wa AFCON 2025 atapata Dola za Kimarekani Milioni 7, ambazo ni takribani Shilingi Bilioni 17.3 za Tanzania. ambayo ni fedha kubwa zaidi katika historia ya michuano hiyo na Mshindi wa pili atajinyakulia Dola Milioni 4, sawa na Shilingi Bilioni 9.96 za Tanzania.

Hivyo  timu zitakazofika nusu fainali, CAF imetenga Dola Milioni 2.5 kwa kila moja, na timu zitakazofika robo fainali zitapata Dola Milioni 1.3 kila timu. Hii ni njia ya kuhimiza timu kushindana kwa bidii ili kufikia hatua kubwa na kuongeza motisha kwao.

Ambapo timu zitakazoshindwa kufika mbali zaidi, ikiwa ni pamoja na zile zitakazomaliza katika hatua ya raundi ya 16, zitapata Dola 800,000 kwa kila moja, ambayo ni sawa na Shilingi Bilioni 1.98 za Tanzania.

Aidha katika michuano ya mwaka huu, Taifa Stars (Tanzania), chini ya kocha Miguel Gamondi, itaanza michuano yake kwa mtihani mkubwa dhidi ya Nigeria, moja ya timu kubwa za soka barani Afrika. Mchezo huu umepangwa kuchezwa Desemba 23 mwaka huukuanzia saa mbili na nusu usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Hata hivyo muundo huu mpya wa zawadi unaonyesha jitihada za CAF kuongeza thamani ya Kombe la Mataifa ya Afrika na kuhimiza ushindani mkali miongoni mwa timu zote. Mashabiki wa soka sasa wanasubiri kwa hamu kuona ni timu gani itapata nafasi ya kutwaa taji la bara la Afrika mwaka 2025.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii