Tanzania, Uganda na Kongo kutupa karata zao AFCON

Wawakilishi wa kanda ya Afrika Mashariki na Kati kwenye michuano ya kandanda kwa mataifa ya Afrika - AFCON 2025, wanatupa karata zao za kwanza uwanjani leo Jumanne.

Baadaye jioni, Taifa Stars ya Tanzania itaitunishia misuli Nigeria kwa mchezo unaotazamiwa kuwa mgumu kwa Stars ambayo imekuwa na historia isiyoridhisha kwenye michuano ya AFCON.

Uganda-the Cranes, wenyewe wanajipanga kwa mtanange na Tunisia itakapotimu saa tatu usiku. Michezo mitatu inasubiriwa kwa shauku kubwa na mashibiki.

Katika michezo mitatu ya jana, Mali iliyo kundi A ililazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wake na Zambia.

Bafana Bafana ya Afrika Kusini iliondoka na alama tatu kwa kuichapa Angola mabao 2-1. Matokeo sawa na hayo yalipatikana pia na Mafarao wa Misri walioilaza Zimbabwe bao 2-1.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii