MWANAMKE ALIYEISHI ZAIDI YA MIAKA 20 BILA FIGO AFARIKI DUNIA

 Asia Mustapha, mwanamke aliyepambana na maradhi ya figo kwa zaidi ya miaka 20 na kutegemea huduma ya kusafisha damu kwa mashine (dialysis), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Desemba 24 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa kipindi chote cha maisha yake, Asia alionyesha ujasiri wa kipekee katika kukabiliana na changamoto kubwa za kiafya, huku akiwa tayari amepoteza wazazi wake wote wawili ambao walikuwa msaada na nguzo muhimu katika safari yake ya matibabu.

Licha ya hali ngumu aliyokuwa akiishi nayo, Asia aliendelea kuwa chanzo cha matumaini kwa wagonjwa wengi na jamii kwa ujumla, wakimchukulia kama mfano wa uvumilivu, imani na mapambano ya maisha dhidi ya maradhi sugu.

Taarifa kutoka kwa familia zinaeleza kuwa mazishi ya marehemu Asia Mustapha yanatarajiwa kufanyika leo saa saba mchana katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo kifo chake kimeacha pengo kubwa kwa familia, marafiki na watu wote walioguswa na safari yake ya maisha yenye mafunzo makubwa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii