Trump atoa onyo kali kwa Makamu wa Rais wa Venezuela

Rais wa Marekani Donald TrumP ametoa kauli kali dhidi ya Makamu wa Rais wa Venezuela Delcy Rodríguez akionyesha msimamo mkali wa Washington kuhusu uongozi wa Caracas.

Katika mahojiano na  vyombo vya habari nchini humo  Trump amesema  kuwa endapo Rodríguez hatofanya maamuzi sahihi basi "atalipa gharama kubwa zaidi" kuliko ile iliyomkuta Nicolás Maduro.

 Hata hivyo  vyombo hivyo  havikufafanua ni swali gani aliloulizwa Trump lililopelekea kutoa kauli hiyo, wala halikueleza alichomaanisha aliposema "maamuzi sahihi."

Haya yanajiri siku chache baada ya Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kukamatwa mnamo siku Jumamosi na kupelekwa Marekani na vikosi maalum vya Marekani.

Maduro anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya uhalifu wa dawa za kulevya na ushirikiano na magenge yaliyotajwa kuwa ya kigaidi.

Baada ya kuondolewa madarakani kwa nguvu, Mahakama ya Juu ya Venezuela ilimteua Makamu wa Rais, Delcy Rodríguez, kuwa kaimu rais hadi uchaguzi mpya utakapoitishwa.

Wakati huo huo, jeshi la Venezuela ambalo ni mhimili muhimu wa mamlaka nchini humo, limeonekana kuonyesha uungwaji mkono kwa Rodríguez.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii