Operesheni ya kumkamata Maduro yasababisha vifo 32

Cuba imethibitisha kuwa raia wake 32 waliuawa wakati wa operesheni ya Marekani ya kumkamata Nicolás Maduro.

Nchi inayoongozwa kikomunisti ambayo inategemea mafuta ya Venezuela - ilikuwa ikisimamia ulinzi wa Maduro na ina maafisa wake katika jeshi la Venezuela.

"Kutokana na shambulio la kihalifu lililofanywa na serikali ya Marekani dhidi ya taifa la Venezuela, Wacuba 32 walipoteza maisha katika mapigano, serikali ya Rais Miguel Díaz-Canel imesema.

Siku mbili za maombolezo zimetangazwa huku Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel akisema ni kwa heshima ya wapiganaji jasiri wa Cuba ambao walivamia magaidi waliovalia sare za kifalme waliomteka nyara na kuwaondoa kinyume cha sheria rais wa Venezuela na mkewe kutoka nchini mwao.

Alipoulizwa kuhusu uwezo wa hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Cuba, Donald Trump amesema hakuna haja hatua kama hiyo kwani kuna uwezekano ikaanguka yenyewe.

Lakini hakupuuza uingiliaji kati kijeshi dhidi ya Colombia, akimtaja rais wake wa mrengo wa kushoto Gustavo Petro kama mlanguzi wa dawa za kulevya na mtu mgonjwa.

Petro amekanusha tuhuma hizo, akimwonya Trump kutomkashifu.

Maduro anatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Marekani leo

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii