Shirika la Wananchi la Amani na Uwiano wa Jamii (CPCC), limesema hivi majuzi kwamba takriban raia 105 kutoka DRC wamefariki dunia katika kipindi cha wiki mbili zilizopita wakiwa kambini huko nchini Burundi wakati huu hali ikiendelea kuwa mbaya zaidi kila uchao.
Kulingana na rais wa kamati kuu ya shirika hilo, Ahadi Bya Masu, vifo hivi vinatokana na ukosefu wa msaada katika suala la makazi, huduma ya afya, na chakula, huku akishangazwa na hali hiyo.
Amesema wamerikodi vifo zaidi ya 105 katika kambi mbalimbali za wakimbizi nchini Burundi, vinavyosababishwa na ukosefu wa malazi ya kutosha, ukosefu wa huduma ya afya, na ukosefu wa usaidizi wa kibinadamu uliopangwa.
Baadhi hata walishambuliwa na watu wenye mishale na silaha zenye nncha kali.
Ahadi Bya Masu alitoa wito kwa serikali ya Kongo na washirika wa kimataifa kutoa msaada wa heshima na endelevu kwa watu hawa waliokimbia uvamizi wa AFC/M23.
Kulingana naye, usaidizi wa kutosha ungewalinda kutokana na vitisho vyovyote zaidi katika kambi za wakimbizi nchini Burundi.
Raia wa Congo ambao hivi majuzi walikimbia vita vya AFC/M23 katika maeneo ya Uvira na Fizi kwa sasa wanahifadhiwa katika kambi za Rugombo, Rumonge, na Gatumba nchini Burundi.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime