Mtoto wa miaka 13 Amnunulia Mama Gari

Kijana mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 13 William Rabillo kutoka Nevada nchini Marekani ametikisa mitandao ya kijamii baada ya kufanikiwa kumnunulia mama yake gari kufuatia kazi ya kukata nyasi aliyoifanya kwa miezi kadhaa ili kuweka akiba.

Rabillo ambaye amekuwa akilea ndoto ya kumsaidia mama yake ambaye ni mzazi pekee (single mother) alitumia mapato yake ya muda mrefu kununua gari lililotumika (used) aliloliona kwenye mtandao wa Facebook Marketplace.

Katika tukio hilo lililokuwa la kusisimua na kugusa hisia kijana huyo alimshangaza mama yake kwa kumpa funguo za gari hilo kama zawadi hatua iliyomwacha mama huyo akiwa ameduwaa kwa furaha na mshangao.

Tukio hilo limepokelewa kwa pongezi na msisimko mkubwa mtandaoni watu wengi wakimsifu kijana huyo kwa moyo wa upendo kujituma na kuthamini juhudi za mama yake.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii