Venezuela haijatishwa na Marekani

Rais wa muda wa Venezuela, Delcy Rodriguez amesisitiza kwamba nchi yake haina hofu yoyote licha ya madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba anaiongoza Venezuela baada ya kumuondoa mtangulizi wake Nicolas Maduro.

Akizungumza katika hafla ya kuwakumbuka Wavenezuela 100 ambao serikali yake inadai waliuawa katika shambulio la Marekani amesema hawajawa chini ya mamlaka ya mtu na wala hajatishwa.

Rodriguez aliongeza kwamba siku ambayo majeshi ya Marekani yalifanya mashambulizi dhidi ya taifa lake Januari 3 hakuna aliyejisalimisha na kulikuwa na mapambano ya kulinda taifa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii