Umoja wa Mataifa amesema Marekani ina ‘wajibu wa kisheria' kuendelea kulipa michango inayofadhili mashirika ya umoja huo hata baada ya Ikulu ya White House kutangaza kujiondoa katika zaidi ya mipango 30 inayoiendesha.
Msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric, amesema kama ambavyo wamekuwa wakisisitiza mara kwa mara michango iliyokadiriwa kwa bajeti ya kawaida ya Umoja wa Mataifa na bajeti ya ulinzi wa amani kama ilivyoidhinishwa na Mkutano Mkuu ni wajibu wa kisheria chini ya umoja huo kuwa nchi zote wanachama zitimize.
Awali Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres alionesha kusikitishwa kutokana na uamuzi wa Trump kujiondoa katika mashirika 31 yanayohusiana na umoja huo ikiwemo shirika la idadi ya watu na mkataba unaoweka masharti ya mazungumzo ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi.
Kadhalika Marekani pia itajiondoa katika mashirika na mipango mingine kadhaa ya kimataifa isiyohusiana na Umoja wa Mataifa.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime