Maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa jeshi la Kongo, waliokamatwa kwa miezi kadhaa iliopita, wameshtakiwa rasmi na tayari wamehamishiwa katika gereza la kijeshi la Ndolo huko Kinshasa.
Mashtaka yao ni makubwa, ikiwa ni pamoja na kula njama za jinai, kupanga njama dhidi ya mkuu wa nchi, kujaribu kuua, na uhaini, kwa madai ya kuwasiliana na taifa la kigeni na wote ni maafisa waliokuwa karibu na rais Felix Tshisekedi.
Miongoni mwa wale wanaolengwa na wimbi hili la kukamatwa ni Jenerali Franck Ntumba, mkuu wa zamani wa Kaya ya Rais ya Kijeshi, huduma iliyounganishwa moja kwa moja na Mkuu wa Nchi.
Pia amejumuishwa Jenerali Christian Tshiwewe, aliyekuwa Mkuu wa majaehsi wa FARDC, na mshauri wa kijeshi wa Rais Félix Tshisekedi wakati wa kukamatwa kwake.
Jina lingine lililotajwa ni Jenerali Christian Ndaywel Okura, aliyekuwa mkuu wa ujasusi wa kijeshi; aliteuliwa kuwa Mkuu wa majeshi ya vikosi vya Ardhini takriban mwaka mmoja uliopita.
Kwa jumla, majenerali wakuu kumi na mmoja na maafisa wakuu wa jeshi kumi na wanne wanaripotiwa kuhusika, kulingana na taarifa zetu. Vyanzo vya ndani ya serikali vinaonyesha kuwa hili ni jaribio la kuvuruga taasisi hizo. Maafisa wengi hawa wanashtakiwa kwa uhaini na kula njama dhidi ya Serikali.
Kesi za kisheria zinaongezeka. Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma kwa sasa inapanga kuskiliza kesi. "Kumekuwa na kuharakishwa kwa mchakato ndani ya mfumo wa haki wa kijeshi," chanzo cha mahakama kinaelezea. "Baadhi watafikishwa mahakamani hivi karibuni," chanzo hicho hicho kinaongeza.
Awamu ya kabla ya kesi imekamilika. Mahojiano mengi yamefanywa. Maafisa wengi hawa walihamishiwa gereza la kijeshi la Ndolo huko Kinshasa wiki moja iliyopita. Wamewekwa rasmi chini ya hati za kukamatwa kwa muda tangu Jumanne.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime