Ibaada ya mazishi ya watu waliouawa katika mapigano yafanyika Goma

Maelfu ya waombolezaji walijitokeza jijini Goma Mashariki ya DRC Januari   8 kuhudhuria ibaada ya mazishi ya watu 22 waliouawa wakati wa mapigano ya hivi karibuni kati ya jeshi la FARDC na waasi wa M23.

Wakati wa hafla hiyo familia za waliouawa ziligubukiwa na huzuni kutokana na uzito wa kuwapoteza wapendwa wao katika mapigano hayo.

Hayo yalijiri wakati mapigano yakiendelea katika Mji wa Masisi ambapo wanajeshi wa DRC wamekuwa wakipambana waasi wa M23 wanaodhibiti mji wa Goma na Bukavu tangu mwaka uliopita.

Jeshi la DRC FARDC na waasi wa M23 wamekuwa wakiendelea kupigana licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano. REUTERS - Arlette Bashizi

Umoja wa Mataifa na serikali ya Kinshasa wanaituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao wa M23 madai ambayo Kigali imeendelea kukanusha.

Mbali na mauaji machafuko mashariki ya Congo yamesababisha mamia kwa maelfu ya raia kukimbia makazi yao, hali ambayo imefanya hali ya kibinadamu kuwa mbaya.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii