Watu wawili wauwawa kufuatia shambulizi la Urusi Kharkiv

Watu wawili wameuliwa katika shambulizi la Urusi lililofanywa katika mji wa Kharkiv mashariki mwa Ukraine ambapo shambulio la Urusi katika mji wa Kharkiv kaskazini mashariki mwa Ukraine limewaua watu wawili na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Taarifa hiyo imetolewa mapema leo na gavana wa mkoa Oleg Synegubov akisema kufikia sasa watu wawili wanajulikana kuuawa na mashambulizi ya adui nje kidogo ya Kharkiv  akiandika kwenye mtandao wa Telegram.

Pia alisema watu wengine watatu walijeruhiwa katika shambulio hilo la usiku kucha huku Urusi imeishambulia Ukraine kwa ndege zisizo na rubani na makombora ya kila siku katika miezi ya hivi karibuni ikilenga miundombinu ya nishati na kukatisha umeme katika kilele cha baridi kali.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii