Serikali ya Somalia imefuta makubaliano yote iliyotia saini na Umoja wa Falme za Kiarabu kuhusiana na mvutano juu ya hatua ya Israel kuitambua Somaliland kama nchi huru.
Somalia imefuta makubaliano yote na Umoja wa Falme za Kiarabu huku kukiwa na mvutano kuhusu utambuzi wa Israeli wa Somaliland.
Katika taarifa yake iliyotolewa hapo jana serikali ya Somalia inaripoti kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu ulitumia ardhi ya Somalia kumsaidia mwanaharakati anayepigania uhuru raia wa Yemen kutoroka nchi yake.
Somaliland ina nafasi ya kimkakati katika Ghuba ya Aden na ina sarafu yake pasipoti na jeshi inayoonekana kama njia muhimu ya kufanyia mashambulizi kwa Israeli kuwalenga waasi wa Houthi nchini Yemen au kwa Umoja wa Falme za Kiarabu kuwapelekea misaada na mahitaji washirika barani Afrika.
Umoja wa Falme za Kiarabu ulijenga na kuendesha bandari kubwa ya maji ya kina kirefu na kituo cha kijeshi huko Berbera, Somaliland.
Serikali ya Somalia imesema Umoja wa Falme za Kiarabu haitaruhusiwa tena kufanya kazi huko Berbera, ingawa ina mamlaka ya kinadharia tu juu ya eneo hilo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime