Trump atangaza ushuru kwa washirika wa kibiashara wa Iran

Rais Donald Trump amesema kuwa nchi yoyote itakayofanya biashara na Iran itatozwa ushuru wa asilimia 25 kufuatia hatua ya Iran kuyakandamiza kwa nguvu kubwa maandamano ya kupinga ugumu wa maisha.

Trump alitoa taarifa hiyo kwa kuandika kwenye jukwaa lake la mitandao ya kijamii  kwamba kuanza mara moja, nchi yoyote inayofanya biashara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran italipa ushuru huo kwa biashara yoyote inayofanywa na Marekani na kwamba amri hii ni ya mwisho.

Hata hivyo nchi ya China, Brazili, Uturuki na Urusi ni miongoni mwa nchi zinazofanya biashara na Iran. Hata hivyo hakuna uwazi kuhusu ikiwa tangazo hilo linawaathiri washirika wote wa biashara au baadhi yao.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii