Díaz-Canel: Hakuna mazungumzo kati ya Cuba na Marekani

Rais wa Cuba Miguel Díaz-Canel amesema mpaka sasa hakuna mazungumzo yoyote ya kutafuta makubaliano na Marekani yanayoendelea kufuatia vitisho vilivyotolewa na rais Donald Trump.

 Miguel Díaz-Canel alisema  hayo Januari 12 mwaka huu kwamba utawala wake hauko kwenye mazungumzo na serikali ya Marekani ikiwa ni siku moja baada ya Rais Donald Trump kutishia kisiwa hicho cha Karibik kufuatia shambulizi la Marekani dhidi ya Venezuela.

Aidha Díaz-Canel alichapisha taarifa nyingi fupi katika mtandao wa kijamii wa X baada ya Trump kupendekeza Cuba "ifanye makubaliano kabla haijachelewa ambapo hukuweka bayana ni aina gani ya makubaliano hayo.

Hata hivyo aliandika kwamba ili "uhusiano kati ya Marekani na Cuba uendelee lazima utegemee sheria ya kimataifa badala ya uadui, vitisho, na kulazimishwa kiuchumi." Kauli zake zilichapishwa tena na Waziri wa mambo ya nje wa Cuba Bruno Rodríguez kwenye mtandao wa X.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii