Myanmar ilifanya mashambulizi ya kikatili dhidi ya jamii ya wachache wa Rohingya kwa lengo la kuiangamiza jamii hiyo Gambia iliripoti taarifa hiyo .
Waziri wa Sheria wa Gambia Dawda Jallow ameiambia mahakama ya kimataifa ya Haki ICJ iliyoko The Hague Uholanzi siku ya jumatatu ikiwa ni wakati wa kuanza kwa kesi ya mauaji ya kimbari.
Hivyo Dawda amesema kuwa mashtaka yao si masuala ya falsafa za sheria bali ni masuala yanayowahusu watu halisi Warohingya waliolengwa kwa maangamizi.
Katika hatua hiyo Gambia ilifungua kesi kwa mara ya kwanza dhidi ya Myanmar mnamo mwaka 2019 ikidai kuwa "operesheni ya kusafisha” iliyofanywa na jeshi la Myanmar mwaka 2017 ilikiuka Mkataba wa kuzuia Mauaji ya Kimbari wa mwaka 1948.
Aidha Uamuzi wa mwisho unaweza kuchukua miezi au hata miaka na ingawa ICJ haina njia ya kutekeleza maamuzi yake, uamuzi unaounga mkono Gambia utaongeza shinikizo zaidi la kisiasa kwa Myanmar.
Hata hivyo Myanmar ambayo kwa sasa ipo mikononi mwa utawala wa kijeshi imekanusha mashtaka dhidi yake hukunUjerumani, Ufaransa na Uingereza zimejiunga na kesi hiyo tangu wakati huo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime