Wanafunzi nchini Iran walifanya maandamano mitaani mjini Tehran Desembe 29 mwaka huu ambapo ni siku moja baada ya wafanyabiashara wa mji mkuu huo kuandamana kupinga hali mbaya ya kiuchumi ambapo mjini Tehran ni karibu na baadhi ya vyuo vikuu huku baadhi ya maduka yaliyofungwa siku iliyopita katikati mwa mji mkuu yakionekana kufunguliwa tena.
Hatua hiyo ya wanafunzi ilijiri baada ya maandamano ya Jumatatu katikati mwa Tehran yaliyofanywa na wamiliki wa maduka na siku moja kabla ya kufungwa kwa muda kwa benki shule na biashara nyingine katika mji huo mkuu na katika majimbo mengi ili kuokoa nishati wakati wa hali ya hewa kali ya baridi.
Aidha Rais Masoud Pezeshkian ambaye ana mamlaka machache chini ya mfumo wa serikali wa Iran kuliko kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei alikutana na viongozi wa wafanyakazi na kutoa mapendekezo ya kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi kulingana na shirika la habari la Mehr.
Hata hivyo uchumi wa nchi hiyo ambao tayari umeathiriwa pakubwa na miongo kadhaa ya vikwazo vya Magharibi ulizidi kuwa mbaya baada ya Umoja wa Mataifa mwishoni mwa Septemba mwaka huu kurejesha vikwazo vya kimataifa vilivyohusishwa na mpango wa nyuklia wa nchi hiyo ambavyo viliondolewa miaka 10 iliyopita.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime