Senegal na Congo zimetuma ujumbe wa nia yao baada ya kupata ushindi wa uhakika katika mechi zao za Kombe la Mataifa ya Afrika - AFCON 2025 ambapo Tanzania na Tunisia zilijikatia tiketi za mwisho za hatua ya mtoano.
Ingawa Senegal ambao ni mabingwa wa AFCON 2021 waliwafunga Benin 3 - 0 katika Kundi D mjini Tanger huku Congo walimaliza wakiwa wa pili katika kundi hilo kwa faida ya mabao baada ya ushindi wa 3 - 0 dhidi ya Botswana mjini Rabat hivyo Senegal, Congo na Benin walikuwa tayari wamejihakikishia nafasi zao za 16 bora za michuano hiyo.
Aidha bao la Feisal Salum ambalo lilisawazisha penalti ya Tunisia liliwapeleka Taifa Stars kuwa katika 16 bora kama moja ya timu bora zilizomaliza nafasi ya tatu kwenye makundi yote sita pia timu ya Angola ambayo ilimaliza ikiwa ya tatu katika Kundi B walikuwa wanaomba msaada wa Tunisia kuipiga Tanzania na mwingine kutoka Nigeria ambayo iliifunga Uganda 3 - 1. Lakini bao la Tanzania likaharibu mahesabu yao jambo lililopelekea Tanzania na Angola zimalize na pointi mbili kila mmoja lakini Tanzania ikafuzu kwa faida ya mabao.
Hivyo Taifa Stars sasa watamenyana na wenyeji Morocco mjini Rabat Jumapili wakati Congo itakabana ko na Algeria mjin Rabat Januari 6 ambapo Tanzania wameweka historia kwa kufuzu hatua ya mchujo kwa mara ya kwanza katika miaka 45 walipocheza mara ya kwanza katika AFCON.
Hata hivyo hawajapata ushindi wowote katika mechi 12 ambazo wamecheza kwenye mashindano manne ya AFCON huku Tunisia ikifuzu katika nafasi ya pili kwenye Kundi C na sasa itachuana na Mali mjini Casablanca Jumamosi.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime