Umoja wa Falme za Kiarabu umesema unaondoa vikosi vyake vilivyobaki Yemen baada ya Saudi Arabia kutaka vikosi hivyo viondoke katika nchi hiyo maskini ya Rasi ya Uarabuni ndani ya saa 24.
kufuatia sharti la Saudi Arabia kutaka vikosi hivyo viondoke ndani ya saa 24 huku mvutano ukiongezeka kuhusu mashambulizi makali yanayofanywa na waasi wanaopigania kujitengaambao wanaungwa mkono na Abu Dhabi.
Wizara ya ulinzi ya Falme za Kiarabu imesema inaviondoa vikosi vya kupambana na ugaidi kwa hiari yake huku Abu Dhabi ilikanusha kuhusika na mashambulizi yanayofanywa na waasi.
Baraza la rais la Yemen na Saudi Arabia ambaye ni hasimu wa UAE katika nchi hiyo maskini zaidi ya Rasi ya Uarabuni wote wametaka wanajeshi wa Falme za Kiarabu waondoke.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio pia alizungumza na mawaziri wenzake wa Saudi Arabia na UAE, ambao wote ni washirika muhimu wa Marekani.
Kabla ya Jumanne alfajiri muungano unaoongozwa na Saudi Arabia unaopambana na waasi wa Houthi wa Yemen ulikuwa umeshambulia shehena ya Falme za Kiarabu katika bandari ya Mukalla, ukisema ilikuwa imebeba silaha kwa ajili ya waasi wanaotaka kujitenga, madai ambayo UAE iliyakana.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime