Januari 3 Sudan watakipiga na Senegal katika mechi ya mwanzo kabisa katika uwanja wa Grand Stade de Tanger na usiku wake kutakuwa na mtanange mkali kati ya Mali dhidi ya Tunisia mjini Casablanca.
Hivyo mechi za hatua ya makundi katika michuano ya kandanda ya mataifa ya Afrika AFCON-2025 zimekamilika hapo jana na timu 16 kufanikiwa kuingia katika hatua ya mtoano ya 16 bora huko nchini Morocco.
Mechi za mtoano zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali kuanzia Januari 3. Sudan watakipiga na Senegal katika mechi ya mwanzo kabisa katika uwanja wa Grand Stade de Tanger ambapo usiku wake kutakuwa na mtanange mkali kati ya Mali dhidi ya Tunisia mjini Casablanca.
Mjini Rabat, siku ya Januari 4 wenyeji Morocco watamenyana na Tanzania ambayo imefika katika hatua hiyo kwa mara ya kwanza katika historia pia kwa upande mwingine Afrika Kusini wataingia dimbani dhidi ya vigogo Cameroon.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime