Serikali ya Gabon imesitisha ushiriki wa timu ya taifa ya soka “The Panthers” na kumfungia mshambuliaji nyota Pierre-Emerick Aubameyang, kufuatia kutolewa kwao kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Hatua hizo zilitangazwa na Waziri wa Michezo, Simplice-Desire Mamboula, baada ya Gabon kufungwa 3–2 na Ivory Coast mnamo Desemba 31, huku wakimaliza mkiani katika kundi lao nchini Morocco baada ya pia kupoteza dhidi ya Cameroon na Mozambique.
Mamboula alieleza kuwa serikali imeamua:
Kuvunja benchi la ufundi,
Kusimamisha timu ya taifa hadi taarifa nyingine,
Kuwafungia Bruno Ecuele Manga na Pierre-Emerick Aubameyang.
Alisema matokeo hayo yalikuwa “aibu” kwa taifa, licha ya Gabon kuanza mechi ya mwisho kwa kuongoza mabao mawili kabla ya kupoteza mchezo.
Aubameyang, aliyewahi kuchezea Arsenal na Chelsea, hakucheza mechi ya mwisho baada ya kurejea Marseille kwa matibabu ya jeraha la paja, akisisitiza kuwa changamoto ndani ya timu “ni kubwa kuliko mchezaji mmoja”.
Kocha Thierry Mouyouma, aliyekuwa kwa zaidi ya miaka miwili, pia ametimuliwa. Serikali nyingi barani Afrika kuchukua hatua kama hizi, matukio ya aina hiyo yamepungua kutokana na msimamo mkali wa Fifa dhidi ya kuingiliwa kwa masuala ya soka na serikali.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime