Boti Ya Wahamiaji Yapinduka Gambia 96 wameokolewa

Serikali ya Gambia imethibitisha kisa cha kusikitisha ambapo Boti iliyokuwa imebeba Wahamiaji zaidi ya 200 imeripotiwa kupinduka usiku wa manane mnamo Desemba 31 ,2025 karibu na Kijiji cha Jinack.

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Gambia, Jeshi la Wanamaji lilianzisha Operesheni ya mara moja ya utafutaji na uokoaji baada ya kupokea taarifa za kuzama kwa Boti.

Ambapo mpaka kufikia sasa hivi, Watu 96 wameokolewa, na 39 wanapokea matibabu katika Hospitali ndogo ya Edward Francis ya Gambia, wakati 57 wako katika kituo cha wanamaji.

Kumi kati ya waliookolewa wako katika hali mbaya. Wakati huo huo, Miili saba imepatikana huku wengine kadhaa wakiwa hawajulikani waliko.

Hata hivyo baadhi ya waathiriwa wanaaminika kuwa sio raia wa Gambia, na Mamlaka inasema juhudi zinaendelea kuthibitisha uraia wao.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii