Wapiganaji saba wauawa katika mashambulizi Yemen

Wapiganaji saba wa kundi la waasi wanaotaka kujitenga wameuawa katika mashambulizi ya angani huku muungano unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen ukijibu mashambulizi makali dhidi ya Baraza la Mpito la Kusini - STC.

Hata hivyo vifo hivyo ni vya kwanza kutokana na mashambulizi ya muungano wa kijeshi tangu kundi linalotaka kujitenga la STC lilipoyateka maeneo ya mikoa ya Hadramawt na Mahra mwezi uliopita.

Saudi Arabia na Falme za Kiarabu kwa miaka mingi zimeunga mkono makundi hasimu katika maeneo yanayoendeshwa na serikali ya Yemen lakini mashambulizi ya STC yameikasirisha Riyadh na kuyaacha madola hayo mawili ya Ghuba yenye utajiri wa mafuta yakiwa katika hali ya kutoelewana.

Mohammed Abdulmalik, mkuu wa wapiganaji wa STC katika jimbo la Wadi Hadramaut na Jangwa la Hadramaut, alisema mashambulizi saba ya angani yaliipiga kambi ya Al-Khasah, na kuua watu saba huku zaidi ya 20 wakijeruhiwa.

 Mashambulizi hayo yalitokea muda mfupi baada ya vikosi vinavyounga mkono Saudi Arabia kuanzisha operesheni ya amaniya kuchukua tena udhibiti wa maeneo ya kijeshi huko Hadramawt.

 Aidha Gavana wa Hadramawt Salem Al-Khanbashi, ambaye pia ni kiongozi wa vikosi vya ulinzi wa taifa vinavyoungwa mkono na Saudia alisema kuwa operesheni hiyo si tangazo la vita wala jaribio la kuongeza mvutano.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii