Iran imedai Marekani inatafuta sababu ya kuingilia kati kijeshi kwa kutumia maandamano ya machafuko ya Wairan wanaopinga hali ngumu ya maisha.
Ambapo serikali ya Iran imeishutumu Marekani kuwa kutafuta kutengeneza kisingizio cha kuingilia kati kijeshi, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia "hatua kali" kuhusu ukandamizaji mbaya dhidi ya maandamano makubwa.
Hatua hiyo imekuja kufuatia ujumbe wa Iran katika Umoja wa Mataifa ulichapisha taarifa kwenye mtandao wa X, ukisema ndoto na sera za Marekani kuelekea Iran zimejikita katika mabadiliko ya utawala, huku vikwazo, vitisho, machafuko yaliyoandaliwa, na vurugu yakitumika kama njia ya kutengeneza kisingizio cha kuingilia kati kijeshi.
Aidha ujumbe huo umeapa kwamba mchezo wa Marekani utashindwa tena. Iran imemtuhumu rais Trump Jumanne kwa kuchochea uvunjifu wa uthabiti wa kisiasa, kuchochea vurugu, na kutishia uhuru wa nchi na usalama wa taifa.
Hata hivyo Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa Amir Saeid Iravani aliandika katika barua yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akisema "Marekani na utawala wa Israeli zinabeba dhamana ya kisheria ya moja kwa moja na isiyopingika kwa vifo vya raia wasio na hatia, hasa miongoni mwa vijana.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime