Idadi ya vifo kufuatia maandamano yanayoendelea kuitikisa Iran imeongezeka na kufikia watu 3,428 hayo ikiwa ni kulingana na shirika la haki za binadamu la Iran.
Maandamano hayo yamezusha pia hali ya wasiwasi baada ya Marekani kutishia kuingilia kati na Iran ikionya kuwa italipiza kisasi huku Marekani imeanza kuwaondoa wanajeshi wake katika kambi zilizopo Mashariki ya Kati huku Uingereza ikitangaza kuufunga kwa muda Ubalozi wake mjini Tehran.
Hata hivyo Rais wa Marekani Donald Trump amesema jana usiku kuwa amepewa "taarifa zenye kuaminika" kwamba mipango ya serikali ya kuwanyonga waandamanaji waliokamatwa imesitishwa.
Aidha Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema kwa sasa hali imedhibitiwa huku akiishutumu Israel kutaka kuiingiza Marekani vitani kwa niaba yake.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime