Afcon: Senegal kuchuana na Morocco kwenye mechi ya fainali

Senegal na wenyeji Morocco ndio wamefuzu hatua ya fainali kwenye mashindano ya Kombe la Afrika AFCON baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali Jumatano usiku.

Simba wa Teranga Senegal waliifunga Misri bao 1-0 bao lililopachikwa nyavuni na Sadio Mané mnamo dakika ya 78 Baadaye Nigeria waliondolewa kwa mbinde na wenyeji Morocco walioshinda kupitia mikwaju ya penati 4 kwa 2.

Hata hivyo Jumamosi Misri na Nigeria zitachuana ili kugombea nafasi ya tatu katika  michuano ya Afcon  huko Casablanca kabla ya mtanange wa fainali kati ya Senegal na Morocco kuchezwa siku ya Jumapili mjini Rabat.

 #10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii