Shughuli ya upigaji kura nchini Uganda imechelewa kuanza katika maeneo mengi ya nchi hali iliyozua wasiwasi miongoni mwa wapiga kura waliowasili mapema vituoni.
Awali vituo vya kupiga kura vilitarajiwa kufunguliwa saa moja asubuhi lakini kufikia saa mbili na nusu asubuhi upigaji kura ulikuwa bado haujaanza katika vituo kadhaa Kulingana na ripoti za awali changamoto kuu inayosababisha kuchelewa huko ni hitilafu za mashine za kuwatambua wapiga kura.
Ambapo ni zaidi ya raia milioni 21 wanatarajiwa kushiriki uchaguzi wa leo ili kuwachagua rais na wabunge katika ripoti iliyotolewa na vyombo vya habari nchini humo vimedai kuwa maafisa wa uchaguzi wamekuwa wakijitahidi kurekebisha matatizo ya kiufundi yanayohusiana na mashine hizo.
Wakati huo huo maafisa wa usalama wamesambazwa katika maeneo mbalimbali nchini huku raia wakiamkia siku ya kupiga kura. Ingawa upigaji kura unaendelea taratibu asubuhi hii wapiga kura tayari wameanza kuwasili katika vituo vyao.
Maafisa wa usalama pia wameonekana wakiondoa picha za wagombea zilizokuwa bado zimebandikwa licha ya kipindi cha kampeni kumalizika. Waandishi wa habari walioko jijini Kampala wameshuhudia uwepo mkubwa wa vyombo vya usalama karibu kila pembe ya jiji wengine wakiwa kwenye magari ya doria na wengine wakizunguka kwa miguu.
Hata hivyo mjini Kampala baadhi ya wakazi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kama kawaida ingawa idadi kubwa ya polisi imeonekana kuwafanya baadhi ya raia kuwa na hofu.
Katika eneo la Soroti hatua kali za kiusalama zimewekwa huku raia wakizuiwa kutoka nje kuanzia jioni. Wakati huohuo mawakala wa vyama mbalimbali vya kisiasa tayari wamewasili katika vituo vya kupiga kura kusimamia zoezi hilo.
Upigaji kura nchini Uganda unatarajiwa kuendelea hadi saa 10 jioni na maafisa wamethibitisha kuwa wapiga kura wote watakaokuwa kwenye foleni kufikia wakati huo wataruhusiwa kupiga kura.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime