Ulaya Yatuma Vikosi Greenland Kusaidia Denmark

Vikosi vya kijeshi kutoka mataifa kadhaa ya Ulaya ikiwemo Ujerumani na Ufaransa vinaendelea kuwasili katika kisiwa kinachojitawala cha Greenland kwa lengo la kuonyesha mshikamano na Denmark kuhusu usalama wa eneo hilo.

Hatua hiyo inakuja baada ya mazungumzo kati ya Marekani Denmark na viongozi wa Greenland kushindikana kufikia makubaliano juu ya mustakabali wa kisiasa na kiusalama wa kisiwa hicho kilichopo katika eneo la Aktiki.

Ambapo maafisa wa Ulaya wamesema uwepo wa wanajeshi hao ni ishara ya kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na kulinda maslahi ya Denmark pamoja na utulivu wa Greenland.

Aidha Greenland ambayo ina umuhimu mkubwa wa kijiografia na kiuchumi imekuwa kivutio cha mataifa makubwa kutokana na rasilimali zake na nafasi yake katika usalama wa Aktiki.

Hata hivyo kwa sasa Denmark na washirika wake wa Ulaya wamesisitiza kuwa wataendelea kuilinda Greenland huku wakitafuta njia ya kidiplomasia kutatua tofauti zilizojitokeza.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii