Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine anaripotiwa kuwekwa katika kizuizi cha nyumbani huku mchakato wa kuhesabu kura za uchaguzi mkuu ukiendelea nchini humo.
Hatua hiyo inakuja wakati matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi yakimuonyesha Rais wa sasa Yoweri Museveni akiongoza kwa kishindo dhidi ya mpinzani wake mkuu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kampala mawasiliano ya Bobi Wine na wafuasi wake yamedhibitiwa huku vikosi vya usalama vikizingira makazi yake hali iliyozua wasiwasi miongoni mwa vyama vya upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu.
Mwandishi wetu Babu Abdallah amezungumza na Emmazel Lubega akiwa Kampala kuhusu hali hiyo wakijadili mazingira ya uchaguzi hatua za kiusalama pamoja na athari zake kwa demokrasia nchini Uganda.
Mazungumzo hayo yanaeleza kwa kina mvutano wa kisiasa unaoendelea wakati taifa hilo likisubiri matokeo kamili ya uchaguzi.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime