Watu saba wauawa katika machafuko Uganda

Takribani watu saba wameuwawa katika machafuko usiku wa kuamkia leo katikati mwa Uganda ikiwa ni siku moja baada ya uchaguzi wa kitaifa ambao unaonekana kumrejesha madarakani Rais Yoweri Museveni kwa muhula mwingine.

Ghasia zimeripotiwa katika maeneo ya Butambala ambako polisi na mbunge wa eneo hilo walitoa maelezo yanayokinzana kuhusu chanzo cha vifo hivyo.

Polisi walisema kundi la wafuasi wa upinzani lilishambulia kituo cha polisi huku mbunge Muwanga Kivumbi akidai kuwa watu waliuawa ndani ya nyumba yake walipokuwa wakisubiri matokeo ya uchaguzi wake.

Matokeo ya awali yanaonyesha Museveni anaongoza kwa zaidi ya asilimia 75 huku mpinzani wake Bobi Wine akidai udanganyifu mkubwa na kutangaza kuwa vikosi vya usalama vilikuwa vimezingira nyumba yake.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii