Mwanasiasa mashuhuri wa Uingereza Peter Mandelson amejiuzulu kutoka chama tawala cha Labour kukwepa kile alichokiita "fedheha zaidi" kufuatia kuibuliwa tena taarifa za urafiki wake na Jeffery Epstein.
Mandelson aliyefukuzwa ubalozi akiwa anaiwakilisha Uingereza nchini Marekani mwaka jana kwa sababu ya mafungamano yake na Epstein yumo kwenye nyaraka zilizochapishwa siku ya Ijumaa na Wizara ya Sheria ya Marekani kuhusiana na mfadhili huyo aliyekufia jela alikotiwa kwa kashfa na ngono na watoto wadogo.
Mandelson amesema jioni ya jana alimuandikia katibu mkuu wa Labour, Hollie Ridley, kuelezea azma yake hiyo, licha ya kudai kuwa tuhuma dhidi yake ni za uongo.
Miongoni mwa mawasiliano yaliyomo kwenye nyaraka hizo yanamuonesha Mandelson akimuhakikishia Epstein kuwa angelipigania suala la mfadhili huyo kulipwa na serikali ya Uingereza huku taarifa za benki zikimuonesha yeye mwenyewe kupokea dola 75,000 kutoka kwa Epstein baina ya mwaka 2003 na 2004.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime