Kupitia taarifa iliyotolewa kwenye tovuti yao rasmi, Ubalozi wa Marekani umekufunzi kufunga ofisi zao katika nchi mbalimbali ikiwemo Burundi, Rwanda, na Uganda.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo imetokana na ukosefu wa fedha unaoikabili Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, baada ya serikali kuu kuchukua hatua za kupunguza matumizi ya fedha nje ya nchi.
Hatua hiyo inakuja wakati Marekani hivi karibuni ilipotangaza kusitisha utoaji wa viza kwa raia wa nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Burundi na nchi nyingine barani Afrika kama sehemu ya mageuzi ya sera za uhamiaji.
Sio tu katika nchi zilizoainishwa hapo juu ambapo mabalozi ya Marekani yamefungwa taarifa zinaonyesha kuwa ofisi za ubalozi pia zimefungwa katika nchi nyingine kama Ethiopia na maeneo mengine.
Aidha, imeripotiwa kuwa mabalozi wa Marekani waliowahi kuhudumu katika nchi hizo wameitwa Washington, D.C. kwa maagizo kutoka Ikulu, moja ya hatua inayowekwa katika muktadha wa sera mpya za utekelezaji.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime