Ryan Routh Afungwa Maisha kwa Jaribio la Kumuua Rais Trump

MAHAKAMA nchini Marekani imemhukumu Ryan Routh kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kumuua Rais wa Marekani, Donald Trump, miezi miwili kabla ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2024.

Tukio hilo lilitokea Septemba 2024 katika Klabu ya Kimataifa ya Gofu ya Trump iliyopo West Palm Beach, jimbo la Florida, wakati Trump akiwa bado ni mgombea wa kiti cha urais.

Kwa mujibu wa mashtaka, Routh alipanga na kutekeleza jaribio hilo kwa nia ya kuhatarisha maisha ya Trump, lakini alizuiwa na vyombo vya usalama kabla ya kufanikisha mpango wake.

Aidha mahakama ilieleza kuwa kosa hilo ni tishio kubwa kwa usalama wa taifa na demokrasia ya Marekani, hivyo kutoa adhabu kali kama fundisho kwa wengine wenye nia kama hiyo.

Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote, jaji aliamua kumpa Routh kifungo cha maisha bila msamaha, akisisitiza kuwa sheria lazima isimame kulinda viongozi na raia kwa ujumla.

Hata hivyo hukumu hiyo imepokelewa kama ujumbe mzito dhidi ya vitendo vya vurugu za kisiasa nchini Marekani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii