Marekani imetaka mazungumzo huku viongozi wa Misri, Eritrea, Somalia na Sudan wakijadili mgogoro wa Tigray. Jeshi la Ethiopia limeripotiwa kuingia Mekelle, huku hofu ya vita vya kikanda ikiongezeka.
Marekani imetoa wito wa kujizuia na kurejea kwenye meza ya mazungumzo, huku mapigano katika eneo la Tigray nchini Ethiopia yakiongeza hofu ya vita kuenea katika Pembe ya Afrika.
Wito huo umetolewa wakati viongozi wa Misri, Eritrea, Somalia na Sudan wakikutana nchini Misri kujadili hali inayozidi kuwa mbaya.
Wakati huo huo, vikosi vya serikali ya Ethiopia vimeripotiwa kuingia Mekelle, mji mkuu wa Tigray, na kutwaa tena uwanja wa ndege wa Alula Aba Nega. Waasi wa TPLF walikuwa wameuteka Septemba 23