Eritrea yatuma wanajeshi wake kaskazini mwa Ethiopia

Vyanzo kadhaa nchini Ethiopia vimethibitisha Eritrea kutuma wanajeshi wake kaskazini mwa nchi hiyo, hali inayotishia kuufanya mzozo wa ndani kuwa wa kikanda.

Kulingana na vyanzo hivyo, wanajeshi wa Eritrea wamewasili katika maeneo ya  Adigrat, karibia Kilomita 115 kaskazini mwa Mji wa Mekelle na walikuwa wakielekea kusini.

Ethiopia inaituhumu Eritrea kwa kuyaunga mkono makundi ya waasi katika ardhi yake ambapo wiki iliopita nchi hizo jirani zilisitisha uhusiani wa kidiplomasia.

Mapigano mapya kati ya  jeshi la serikali ya Ethiopia na wapiganaji wa TPLF yalizuka Septemba 23 na kuibua wasiwasi wa uwezekano wa kurejelewa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoshuhudiwa kati ya mwaka wa 2020-2022.

Eritrea inaelezwa kuwa na hofu kuwa  Ethiopia inapanga kuchukua njia ya kuingia kwenye bandari ya shamu, wachambuzi wa masuala ya kimataifa wakisema hatua ya kutuma wanajeshi Ethiopia inalenga kuzuia vita kufika katika himaya yake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii