Harmonize Avunja Rekodi Youtube, Apata Views Mil 1.3 Ndani ya Sekunde 34

STAA wa muziki na CEO wa Konde Gang, Harmonize  usiku wa kuamkia leo Aprili 13, 2022 amevunja rekodi ya Youtube kupitia video yake mpya ya Mdomo aliyomshirikisha msanii wa lebo yake Ibraah kwa kupata watazamaji Milioni 1 na laki 3 ndani ya Sekunde 34.

Video hiyo baada ya kuachiwa katika mtando wa Youtube ilitazamwa zaidi ndani ya muda mfupi na kuvunja rekodi iliyowekwa na kundi la wasanii kutoka Korea Kusini ‘BTS’.

Awali rekodi hii ilikuwa ilishikiliwa na BTS ambao video yao ya ‘Butter’ Mwezi Mei 2021 ilienda trending na kupata Views Milioni 108.2 ndani ya saa 24. BTS walivunja rekodi ya BLACKPINK ya kupata views milioni 86.3 ndani ya saa 24 mwaka 2020.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii