Nchi ambayo watu hawapigi kura

Wabunge wapya wa Somalia wanatarajiwa kuapishwa hivi karibuni kufuatia uchaguzi wa aina yake wa bunge la nchi hiyo, unaojulikana kama 'bunge la watu'.

Lakini watu hawakupiga kura katika uchaguzi ambao umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu takribani miezi minne sasa, ikilinganishwa na zaidi ya mara mbili ya muda uliochukuliwa na India, katika uchaguzi wake uliohusisha watu wengi zaidi duniani, ambapo zaidi ya watu milioni 600 walipiga kura.

Nchi ya Somalia imetumia watu wachache waliopo bungeni ambao walipiga kura na kuwakilisha taifa lenye watu wapatao milioni 16.3.

Hii ni kwa sababu Somalia inatumia mfumo mgumu na usio wa moja kwa moja wa kisiasa na vyama vya siasa havishiriki uchaguzi. Wala uchaguzi wa mtu mmoja kupiga kura haufanyiki.

Badala yake, Baraza la Watu 275 huchaguliwa na wajumbe walioteuliwa na wazee wa koo na wanachama wa mashirika ya kiraia ambao huchaguliwa na maafisa wa serikali wa eneo. Kisha Wabunge wanampigia kura rais, ambaye atakua kiongozi wa nchi.

Wanachama 54 wa bunge dogo na Seneti wanaowakilisha majimbo matano ya Somalia, wanashiriki katika kura ya urais.

Inaonyesha nguvu za koo nchini Somalia , inaunda uti wa mgongo wa jamii ambayo demokrasia ya mtindo wa Magharibi haijakita mizizi.

Pia wanaziba mwanya ulio
Kutokana na na kukosekana kwa serikali yenye nguvu. Somalia haijapata kuwa na serikali thabiti tangu utawala wa kisoshalisti ulioongozwa na Siad Barre ulipoanguka mwaka 1991.

Kutokana na ushindani mkubwa kati ya koo za Somalia, mfumo huo unatokana na kanuni ya kugawana madaraka, ambapo koo kuu nne zina idadi sawa ya viti vya ubunge na koo zilizosalia zimeunganishwa na kupewa nusu ya idadi.

Hii inawafanya wawakilishi wa koo za Somalia kuwa wafalme wa kisiasa.

Wengi wao wanatarajiwa kuapishwa kama wabunge siku ya Alhamisi, kufuatia uchaguzi wa mabaraza mawili ya bunge.

Lakini uchaguzi katika baadhi ya mikoa bado haujahitimishwa kwa sababu ya migogoro ya masuala mbalimbali, ikiwamo uhalali wa wagombea.

Hata hivyo, hii haiwezekani kuchelewesha kuapishwa kwa wabunge wengine.

Uchaguzi ulitikiswa na ufisadi mkubwa, matumizi mabaya ya madaraka na kupuuza sheria za uchaguzi. Inaaminika mamilioni ya dola yalitumika kununua wajumbe katika baadhi ya matukio.

Kwa bahati mbaya, nchi haina taasisi zinazoweza kuchukua hatua dhidi ya ufisadi.

Qatar ni mhusika mkuu katika ulingo wa kisiasa. Wachambuzi wanaamini kuwa ilifadhili kwa mkono mmoja kampeni ya Rais wa sasa Mohamed Abdullahi Farmajo katika kura ya mwaka 2017, na ilikuwa na ufikiaji mkubwa kwa utawala wake.

Shinikizo kubwa la umma lipo kwa bunge kuchukua hatua haraka kumchagua rais mpya, kwani muhula wa rais Farmajo uliisha mnamo Februari 2021.

Lakini alibaki madarakani kwa sababu mabishano ya kisiasa na ukosefu wa maandalizi ulichelewesha uchaguzi wa wabunge, na kumuacha yeye na wabunge bila mamlaka ya kutawala.

Uchaguzi wa bunge hatimaye ulifanyika chini ya shinikizo kutoka kwa wafadhili wa Magharibi ikiwa ni pamoja na Marekani ambayo ilizuia visa kwa maafisa wanaoonekana kuhujumu mchakato wa uchaguzi.

Shirika la Fedha Duniani (IMF) lilisema linaweza kusitisha msaada wa kifedha kwa Somalia ifikapo katikati ya Mei ikiwa uchaguzi hautakamilika.

Mara baada ya serikali mpya kuchukua madaraka, italazimika kushughulikia changamoto za Somalia - ikiwa ni pamoja na ukame. Ukame umekuwa mbaya zaidi katika miaka mitatu iliyopita na mashirika ya misaada sasa yanaonya juu ya njaa.

Zaidi ya watu milioni 3.5 wanahitaji msaada wa chakula, na watoto milioni 1.4 wanakabiliwa na utapiamlo mkali.

Hofu hiyo ilionyeshwa hadharani na Rais wa nchi jirani ya Djibouti Omar Guelleh mwaka wa 2020, aliponukuliwa akisema: "Ninahofia tutaishia kuwa na bunge linalodhibitiwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja na al-Shabab kwa sababu watakuwa wamenunua uungwaji mkono na baadhi ya wabunge. "

Baadhi ya wachambuzi walihisi Bw Guelleh alikuwa akitia chumvi uwezekano wa al-Shabab kupata udhibitoi bungeni, lakini hakuna shaka kwamba wana ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini Somalia.

Watu wenye ushawishi wa kisiasa nchini Somalia walikubaliana muda mrefu uliopita kwamba kura ya mtu mmoja ingefanyika ifikapo mwaka huu, lakini walishindwa kutimiza ahadi hiyo.

Hilo halikushangaza, kwani baadhi ya matakwa muhimu - ikiwa ni pamoja na usajili wa vyama vya siasa na kupitishwa kwa katiba mpya kupitia kura ya maoni - hayakufanyika.

Haijulikani ni kwa kiwango gani kitakuwa kipaumbele cha serikali ijayo, ambayo itakuwa na changamoto nyingi sana

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii